[Hili ni toleo la hati hii kutoka 17 Oktoba 2019.]
BUNGE LA AFRIKA,LIKIZINGATIA Ibara ya 17 ya Mkataba Anzilishi wa Umoja wa Afrika, ulioanzisha Bunge la Afrika ili kuhakikisha "ushiriki kikamilifu wa watu wa Afrika katika maendeleo na utangamano wa kiuchumi wa bara";LIKIZINGATIA PIA Ibara ya 3 (a), (f), na (k) ya Mkataba Anzilishi wa Umoja wa Afrika unaoeleza malengo ya Umoja ili kuwa na umoja na mshikamano mkubwa miongoni mwa nchi za Afrika na watu wa Afrika; kuendeleza amani, usalama na utulivu barani na kuimarisha ushiriki katika mawanda yote ya shughuli za binadamu ili kuinua hali ya maisha ya watu wa Afrika;LIKIZINGATIA ZAIDI Ibara ya 3 ya Protokali ya Mkataba Anzilishi wa Jumuiya ya Uchumi ya Afrika inayohusiana na Bunge la Afrika, ambayo inawezesha utekelezaji kikamilifu wa sera na malengo ya Umoja wa Afrika; kukuza kanuni za haki za binadamu na demokrasia barani Afrika, na kukuza amani, usalama na utulivu;LIKIREJEA Ibara ya 20 ya Mkataba Anzilishi ambayo pia inarejewa kwenye Ibara 9 ya Protokali ya Marekebisho ya Mkataba Anzilishi ya mwaka 2003; na Ibara ya 2 ya Protokali ya mwaka 2002 inayohusiana na Uanzishwaji wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika kama "chombo kinachosimamia uamuzi wa kuzuia, kusimamia na kutatua migogoro";LIKIREJEA Lengo la 4 la Ajenda 2063 ambalo linalenga kuwa na Muundo wa Amani na Usalama unaofanya kazi kikamilifu barani Afrika (APSA) kwa ajili ya kulinda amani, usalama na utulivu barani Afrika;LIKITAMBUA kwamba Ibara ya 18 ya Protokali inayohusiana na Kuanzishwa kwa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika inayoeleza kufanya kazi kwa karibu na Bunge la Afrika katika kuendeleza amani, usalama na utulivu katika Afrika na kulipa kazi ya kuwasilisha ripoti kwa Bunge la Afrika ambazo zitaliwezesha Bunge kutekeleza majukumu yake yanayohusiana na kudumisha amani, usalama na utulivu barani Afrika;LIKITAMBUA KWA MASIKITIKO kuwa ugaidi na siasa kali vinaendelea kuchochewa kwa kuenea, kusambaa na usafirishaji haramu wa silaha ndogo na silaha nyepesi, hali inayotishia amani na usalama barani na kudhoofisha juhudi za kuboresha viwango vya maisha ya watu wa Afrika;LIKITAMBUA kwamba bara la Afrika lina historia ndefu ya migogoro ya silaha na ahadi ya Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika ya kukomesha mapigano ifikapo 2020;LIKITAMBUA jitihada na ushirikiano wa Baraza la Amani na Uslama pamoja na BA katika kukomesha migogoro barani Afrika;LIKISHAWISHIWA kwamba changamoto za amani na usalama zinaweza kutatuliwa tu kupitia juhudi za vyombo vyote vya Umoja wa Afrika;KWA MUJIBU WA ya Kanuni 5 (b), (c) na (d) ya Kanuni za Uendeshaji wa Bunge la Afrika, ambayo pamoja na mambo mengine, inalipa BA madaraka ya kuandaa mijadala, kujadili, kutoa maoni, kutoa mapendekezo kuhusiana na malengo na jambo lolote linalohusiana na Umoja wa Afrika na vyombo vyake, Jumuiya za Uchumi za Kanda, Nchi Wanachama na vyombo na taasisi zake;SASA LINAAZIMIA:5.KUUOMBA Uongozi wa Bunge la Afrika kupitia kwa Rais wa BA, kushauriana na Baraza la Amani na Usalama kuboresha uhusiano na ushirikiano kuhusu masuala ya amani na usalama, ikiwa ni pamoja na kuunda tume ya pamoja ya kutafuta ukweli wa mambo na Kamati ya Ushirikiano, Uhusiano wa Kimataifa na Usuluhishi wa Migogoro ili kwenda katika maeneo yenye migogoro;6.PIA KUIOMBA Kamati ya Ushirikiano, Uhuhisiano wa Kimataifa na Usuluhishi wa Migogoro kufanya ziara za tume huru za kutafuta ukweli wa mambo ili kuongeza uelewa wao kuhusu sababu za migogoro katika bara na kulitaarifu bunge ipasavyo.7.KUOMBA ZAIDI Kamati ya Ushirikiano, Uhusiano wa Kimataifa na Usuluhishi wa Migogoro kutekeleza shughuli zinazolenga kuendeleza ukomeshaji wa mapigano na Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika;Limepitishwa Midrand, Afrika Kusini17 Oktoba 2019