[Hili ni toleo la hati hii kutoka 17 Oktoba 2019.]
Bunge la Afrika,Likizingatia Ibara ya 17 (1) ya Mkataba Ulioanzisha Umoja wa Afrika ambao ulianzisha Bunge la Afrika ili kuhakikisha ushiriki kamili wa watu wa Afrika katika maendeleo na ushirikiano wa kiuchumi wa bara;Likizingatia pia Ibara ya 3 ya Mkataba Ulioanzisha Umoja wa Afrika, ambapo malengo yake, pamoja na mambo mengine, ni kuharakisha muungano wa kisiasa, kijamii na kiuchumi wa bara la Afrika; kukuza ushirikiano wa kimataifa, kwa kuzingatia Mkataba wa Umoja wa Mataifa na Azimio la Dunia la Haki za Binadamu; kuhamasisha maendeleo endelevu kwenye masuala ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni, na pia kuunganisha uchumi wa Afrika; kuratibu na kuoanisha sera miongoni mwa jumuiya za uchumi za kanda zilizopo na za siku za baadaye kwa lengo la kufikia hatua kwa hatua malengo ya Umoja wa Afrika; Likizingatia pia Ibara ya 3 ya Protokali ya Mkataba ulioanzisha Jumuiya ya Uchumi ya Kanda inayohusiana na Bunge la Afrika na ibara ya 4 (a) ya Kanuni za Undeshaji wa Bunge la Afrika ;Likizingatia umuhimu wa nishati kwenye ukuaji jumuishi kwa ajili ya maendeleo ya Afrika;Likizingatia pia kiwango cha chini cha uwekezaji katika sekta ya nishati katika nchi nyingi za Afrika;Likizingatia pia kutokuwepo kwa sera thabiti ya nishati pamoja na kutokuwepo kwa mfumo wa kisheria barani Afrika;Likiamini kuna haja ya kutekeleza programu za UNIDO kuhusu maendeleo ya viwanda barani Afrika;Kwa mujibu wa Ibara ya 5 al. D ya Kanuni za Uendeshaji wa Bunge la Afrika, ambayo inalipa mamlaka ya kutoa mapendekezo na maazimio kuhusu masuala yote yanayohusiana na Umoja wa Afrika na vyombo vyake, Jumuiya za Uchumi za Kanda na vyombo vyao, kwa Nchi wanachama na vyombo na taasisi zao;Sasa linaazimia:1.Kutangaza upatikanaji wa nishati kwa wote kwa bei nafuu na mabadiliko kwenye sekta ya nishati na kuhakikisha upatikanaji wa nishati mbadala kwa wote ifikapo mwaka 2040;2.Kutoa mafunzo kwa rasilimali watu katika ngazi ya chini kuhusiana na masuala ya nishati na kusaidia maendeleo yao, kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa nishati mbadala;3.Kuhimiza nchi wanachama kutumia sehemu kubwa ya bajeti zao kwa ajili ya nishati mbadala;4.Kuanzisha utaratibu wa kukusanya fedha kwa ajili ya nishati mbadala;5.Kutoa misamaha ya ushuru kwa vifaa vinavyotumia nishati mbadala;6.Kuanzisha sera madhubuti ya nishati katika nchi za Afrika;7.Kuhimiza na kusaidia mipango ya nishati ya kikanda;8.Kuhimiza uwekezaji wowote unaohusiana na nishati mbadala;9.Kusisitiza umuhimu wa utekelezaji mzuri wa lengo namba 05 la Malengo ya Maendeleo Endelevu (kuweka usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake na wasichana wote);10.Kuhimiza ubia kati ya sekta ya umma na binafsi katika uwekezaji kwenye nishati;11.Kuanzisha mtandao wa wabunge unaohusika na matumizi ya nishati mbadala;12.Kuandaa sheria ya mfano ya nishati mbadala.Limepitishwa Midrand, Afrika KusiniTarehe 17 Oktoba 2019