[Hili ni toleo la hati hii kutoka 17 Oktoba 2019.]
Bunge la Afrika,IKIZINGATIA Ibara ya 17 ya Mkataba Anzilishi wa Umoja wa Afrika ulioanzisha Bunge la Afrika ili kuhakikisha "ushiriki kamili wa watu wa Afrika katika maendeleo na ushirikiano wa kiuchumi wa bara";LIKIZINGATIA PIA, Ibara ya 3 ya Protokali ya Mkataba Ulioanzisha Jumuiya ya Uchumi ya Kanda inayohusiana na Bunge la Afrika, na Kanuni ya 4 (a) ya Kanuni za Uendeshaji wa Bunge la Afrika, inayolipa BA mamlaka ya kuwezesha ushirikiano wa kanda, maendeleo na uhimizaji wa "kujitegemea kwa pamoja na kufufua uchumi" wa Umoja wa Afrika;LIKIZINGATIA ZAIDI Ibara ya 11 (3) ya Protokali ya BA na Kanuni ya 4 (1) (d) & (e) ya Kanuni za Uendeshaji wa BA, ambayo inalipa BA mamlaka ya kufanya kazi ya uoanishaji au uratibu wa sheria za Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika, pamoja na mambo mengine, kupitia kupendekeza na kuandaa sheria za mfano;LIKIZINGATIA ZAIDI Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za watu wenye Ulemavu, na na katika kutumia njia mifumo ya kijamii na kitababu, ambazo zinahakikisha haki sawa kwa watu bila kujali hali zao, ikiwemo ulemavu;LIKIKUMBUKA ZAIDI, Azimio la BA kuhusu Sheria ya Mfano ya Ulemavu barani Afrika, ambalo lilipitishwa wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Tano, mwezi Oktoba 2018;LIKITAMBUA kwamba watu wenye ulemavu wanakabiliwa na ubaguzi na vikwazo ambavyo vinawazuia kushiriki katika maisha ya kijamii kwa usawa na wengine, wananyimwa haki zao za kuishi kwa uhuru katika jamii pamoja na ulinzi wa kijamii;LIKIKARIBISHA ushirikiano kati ya Bunge la Afrika na Muungano wa Watu wenye Ulemavu Afrika katika kutimiza haki za binadamu kwa watu wenye ulemavu kwa kukuza na kujumuisha ulemavu ndani ya Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika kupitia uandaaji wa Sheria ya Mfano ya Ulemavu;LIKITHAMINI michango kutokana na mashauriano ya kanda kuhusu Rasimu ya Sheria ya Mfano ya Ulemavu ambayo inatoa fursa kwa raia wa Afrika, mashirika ya ngazi ya chini na wadau wengine wenye nia kujihusisha na rasimu ya Sheria ya Mfano;LIKITHAMINI PIA pia msaada wa kitaalamu uliotolewa na Muungano wa Watu wenye Ulemavu Afrika kwa Bunge la Afrika katika kuandaa na kushauriana kuhusu rasimu ya sheria ya mfano ya ulemavu, ambayo itawezesha kutumika katika nchi kwa Protokali ya Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu kuhusiana na Haki za Watu wenye Ulemavu pamoja na kutunga sera na sheria za taifa za haki za binadamu kuusu ulemavu;LIKIAMINI kwamba mfumo wa sheria wa ara ulio kamili na jumuishi wa kusaidia kukuza na kulinda haki za watu wenye ulemavu utatoa mchango mkubwa katika kurekebisha udhaifu mkubwa wa mazingira magumu ya kijamii ya watu wenye ulemavu na kukuza ushiriki wao katika nyanja za kiraia, kisiasa, kiuchumi, kijamii, na kuitamaduni, katika ngazi zote za kitaifa na kimataifa;KWA MUJIBU WA Kanuni ya 5 (b), (c) na (d) ya Kanuni za Uendeshaji wa Bunge la Afrika, ambayo, pamoja na mambo mengine, inalipa BA mamlaka ya kuandaa mjadala, kujadili, kutoa maoni, kutoa mapendekezo na kuchukua maazimio kuhusu malengo na masuala yoyote yanayohusiana na Umoja wa Afrika na vyombo vyake, Jumuiya za Uchumi za Kanda, Nchi Wanachama na vyombo na taasisi zao;SASA LINAAZIMIA:1.KUPITISHA Sheria ya Mfano ya Ulemavu;2.LINAOMBA Uongozi wa BA kuwasilisha Sheria ya Mfano ya Ulemavu kwa Vyombo vya Sera vya UA kwa ajili ya kuidhinishwa na kutumiwa na Nchi Wanachama wa UA.3.KUTEKELEZA shughuli za uhamasishaji kwa ajili ya uridhiaji wa Protokali ya Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu unaohusiana na Haki za Watu wenye Ulemavu na kuidhinishwa na kutumiwa na Nchi Wanachama wa UA;4.KUIMARISHA ushirikiano na kujadiiana kati ya bunge za kanda na kitaifa, kwa lengo la kuongeza uwezo wa wabunge wa kufuatilia na kukuza ujumuishaji wa ulemavu katika sera na mipango ya kitaifa, pamoja na vyombo vya bajeti na sheria.Limepitishwa Midrand, Afrika Kusini17 Oktoba 2019