[Hili ni toleo la hati hii kutoka 17 Oktoba 2019.]
BUNGE LA AFRIKA,LIKIZINGATIA Ibara ya 17 ya Mkataba Anzilishi wa Umoja wa Afrika ulioanzisha Bunge la Afrika ili kuhakikisha "ushiriki kamili wa watu wa Afrika katika maendeleo na ushirikiano wa kiuchumi wa bara";LIKIZINGATIA pia Ibara ya 3 ya Protokali ya Mkataba Ulioanzisha Jumuiya ya Uchumi ya Kanda inayohusiana na Bunge la Afrika, na Kanuni ya 4 (a) ya Kanuni za Uendeshaji wa Bunge la Afrika, inayolipa BA mamlaka ya kuwezesha ushirikiano wa kanda, maendeleo na uuhimizaji wa "kujitegemea kwa pamoja na kufufua uchumi" wa Umoja wa Afrika;LIKIZINGATIA ZAIDI Ibara ya 11 (3) ya Protokali ya BA na Kanuni ya 4 (1) (d) & (e) ya Kanuni za Uendeshaji wa BA, ambayo inalipa BA mamlaka ya kufanya kazi ya uoanishaji au uratibu wa sheria za Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika, pamoja na mambo mengine, kupitia kupendekeza na kuandaa sheria za mfano;LIKIKUMBUKA Azimio la BA kuhusu kuandaa Sheria ya Mfano ya Usalama wa Chakula na Lishe katika Afrika, ambalo lilipitishwa wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Tano, mwezi Oktoba 2018;LIKITAMBUA kwamba nchi nyingi za Afrika ni wadau katika mikakaba ya kimataifa inayohusu usalama wa chakula na lishe (FSN), kama vile Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Uchumi, Jamii na Utamaduni, na kwamba haki ya chakula cha kutosha imeelezwa wazi katika Katiba za Kitaifa za nchi nyingi barani Afrika;LIKIZINGATIA kwamba sera na mifumo ya FSN iliyowekwa katika sheria inafaa zaidi na inakuza uboreshaji endelevu wa FSN, na umuhimu wa kushughulikia changamoto za kimuundo, sera maalumu, programu, sheria na mazingira ya kuwezesha FSN;LIKIZINGATIA uwasilishaji wa rasimu ya Sheria ya Mfano ya Usalama wa Chakula na Lishe, ambayo inazingatia hali mtambuka na ya sekta mbalimbali ya FSN na mitazamo tofauti ya utaratibu wa kisheria za Mataifa ya Afrika;KWA MUJIBU WA Kanuni ya 5 (b), (c) na (d) ya Kanuni za Uendeshaji wa Bunge la Afrika, ambayo, pamoja na mambo mengine, inalipa BA mamlaka ya kuandaa mjadala, kujadili, kutoa maoni, kutoa mapendekezo na kuchukua maazimio kuhusu malengo na masuala yoyote yanayohusiana na Umoja wa Afrika na vyombo vyake, Jumuiya za Uchumi za Kanda, Nchi Wanachama na vyombo na taasisi zao;SASA LINAAZIMIA:1.KURIDHIA rasimu ya kwanza ya Sheria ya Mfano ya FSN barani Afrika;2.KUIOMBA Kamati ya Kilimo kufanya mashauriano ya kikanda kuhusu Rasimu ya Sheria ya Mfano ya FSN katika Afrika, ili kuunganisha michango kutoka kwa raia wa Afrika, mashirika ya ngazi ya chini na wadau wengine wenye nia;3.Inakaribisha msaada wa kitaalamu kutoka FAO na ushirikiano wenye manufaa kati ya PAPA-FSN, Kamati ya Uchumi Vijijini, Kilimo, Maliasili na Mazingira, Ushirikiano mpya wa Shirika la Maendeleo Afrika (NEPAD), na Idara ya Kamisheni ya Uchumi Vijijini Afrika na Kilimo, kwa uandaaji wa Rasimu ya Sheria ya Mfano ya FSN.Limepitishwa Midrand, Afrika Kusini17 Oktoba 2019